Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Abu Hussein al-Hamidawi, Katibu Mkuu wa Kata’ib Hizbullah ya Iraq, siku ya Jumapili (tarehe 5 Bahman 1404 H.S), alitangaza katika tamko lake kwamba kundi hili linazitaka nguvu zote za kijihadi duniani kujiandaa kwa “vita vya jumla” kuiunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Akiashiria kwamba leo nguvu potofu na Wazayuni duniani wamekusanyika kwa lengo la kuilazimisha Iran ijisalimishe, alisisitiza: Vita dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu havitakuwa “ziara ya starehe”. Katika vita kama hivyo, maadui wataonja mauti ya kutisha, na hakuna athari wala mabaki yao yatakayobaki katika eneo hili.
Katibu Mkuu wa Kata’ib Hizbullah ya Iraq, akisisitiza kwamba Iran ni “ngome imara na chanzo cha heshima ya Umma wa Kiislamu”, alisema: Nchi hii kwa zaidi ya miongo minne imesimama pamoja na wanyonge na katika kutetea haki za Umma wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani ziwe juu yake na juu ya Aali zake), bila kubagua misingi ya madhehebu, kabila au rangi.
Akizungumza na vikosi vilivyo chini ya uongozi wake, alisema: Ndugu wapiganaji wanapaswa kuwepo katika uwanja wa mapambano na wajiandae kufikia mojawapo ya mema mawili (yaani ushindi au shahada).
Al-Hamidawi, mwishoni, akirejelea nafasi ya wanazuoni wakuu wa dini, aliongeza: Hasa iwapo wanazuoni wakuu watatoa hukumu ya jihadi ya kuingia katika “vita hivi vitukufu”, basi katika hali hiyo, hukumu au hatua zote za kijihadi—hata zile zitakazofikia kiwango cha “operesheni za kujitoa mhanga”—zitakuwa wajibu kwa ajili ya kuwatetea Waislamu na kulinda uwepo wao.
Maoni yako